Loading...

6/13/2019

Wachezaji wa Liverpool wapewa simu za Iphone X zenye dhamani ya Tsh. Milioni 11


Kila mchezaji na watu wote wa benchi la ufundi la klabu ya Liverpool wamepewa zawadi ya simu aina ya Iphone X yenye uzito wa dhahabu wa 24k yenye thamani ya £3,500 ambazo ni sawa na milioni 11.5 za kitanzania ikiwa ni motisha ya kuwa mabingwa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa Champions League) msimu wa 2018/19. Kwa wachezaji kila simu ina jina na namba ya mchezaji.

Ni takribani miaka 14 tangu klabu ya soka ya Liverpool bila kuwa na taji la UEFA, Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatimae Juni 1, mwaka huu walifanikiwa kutwaa taji hilo katika fainali za michuano hiyo.


Loading...