Loading...

6/14/2019

Watu 47 wauawa katika mashambulizi ya silaha

Watu 47 wameuawa katika mashambulizi ya silaha katika eneo la Niger Magharibi Nigeria.

Mkurugenzi wa Shirika la Usimamizi wa Dharura la Nigeria (SEMA) katika Jimbo la Niger Garrba amesema kuwa vijiji vya Kwaki, Ajatayi, Gwassa, Barden Dawaki, Gyammamiya na Alewa vimeshambuliwa kwa silaha na watu wasiojulikana.

"Kwa sasa miili 47 imepatikana na wengi wamejeruhiwa," alisema.

Garba amesema kuwa karibu watu 2,000 wameyakimbia makazi yao.

Garba alisema kuwa waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu na kwamba uchunguzi umeanza.
Loading...