Waziri Kalemani: Magari mapya ya Wizara ya Nishati kutumia gesi badala ya mafuta


Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amesema lengo la uamuzi huo ni kubana matumizi ya mafuta, kutunza mazingira na kuhamasisha wizara nyingine na watu binafsi kutumia gesi

“Hatuwezi kuhamasisha wengine, tunaanza sisi kwa sababu ni gharama nafuu na inahifadhi mazingira, nitumie nafasi hii kuwaomba Watanzania kuanza kunufaika na gesi yetu ya hapa nchini” alisema Waziri Kalemani.

Aidha, Aprili 2019 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, lilianza mazungumzo na mradi wa mabasi yaendayo kasi ili kuyawezesha mabasi hayo kutumia nishati ya gesi.

Kanuni za bei ya gesi asilia za mwaka 2016, zinaonyesha matumizi ya gesi hiyo katika magari husaidia kuokoa asilimia 40 ya gharama inayotumika katika ununuzi ya lita moja ya bei ya petroli na dizeli ya wakati husika.