Waziri Kigwangalla mgeni rasmi makabidhiano ya Tuzo hii


Na Timothy Itembe, Mara

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla anatarajiwa kuwa mgeni Rasimi katika makabidhiano ya Tuzo ya uhifadhi bora mkoani Mara siku mbili zijazo.

Mkuu wa mkoa Mara, Adamu Kigoma Malima alisema juzi ndani ya  kikao maalumu cha halmashauri ya wilaya Tarime vijijini kilicho washirikisha madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo kuwa wanategemea kuwa na mgeni rasimi Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala katika makabidhiano ya Tuzo ya uhifadhi Bora serengeti.

Malima alisema kuwa ni matarajio yake kuwa jamii ya watu wa Mara watahudhuria makabidhiano hayo ili kupata ujumbe wa mgeni rasimi juu ya utunzaji na uhifadhi wa Mbuga za wanyama zinazotuzunguka lengo ni kuhakikisha kuwa tunawatunza na kuwalinda wanyama wetu kwa maendeleo ya vizazi vijavyo.

Pia Malima alisisitiza kuwa viongozi ngazi ya vijiji na madiwani wanaozunguka Mbuga za Serengeti wanatakiwa kuwepo kwasababu ya kupokea ujumbe utakao tolewa ili kujipanga na uhifadhi bora wa Mbuga za wanyama na kuongeza kasi ya utalii.


Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime Vijijini,Apoll Tindwa alimhakikishia Malima kuwa atagarimia madiwani wake pamoja na watumishi kufuika katika eneo husika na kupokea ujumbe kwalengo la kuja kuwa mabalozi na kueneza ujumbe wa mgeni rasimi kwa jamii ambayo haitakuwa imefika katika makabidhiano hayo.


Tindwa alisema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa ambao kazi yao ni kupinga kila jambo zuri la serikali kwa hali hiyo wanatakiwa kuwalinda wanyama kwasbabu wanyama wanatakiwa kusemewana na kulindwa na Binadamu siovinginevyo.