https://monetag.com/?ref_id=TTIb Waziri mpya wa Viwanda na Biashara aapishwa, anena mazito Ikulu | Muungwana BLOG

Waziri mpya wa Viwanda na Biashara aapishwa, anena mazito Ikulu


Waziri Mteule wa Viawanda na Biashara, Innocent Bashungwa amemuahidi Rais Magufuli kufanya kazi usiku na mchana katika Wizara hiyo.

Bashungwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kuendelea kumpa heshima na kumuamini, huku akiwapongeza viongozi wengine Wateule walioapishwa leo.

"Kwanza nikupongeze Rais kwa Mkutano wa wafanyabiashara ulioufanya juzi niliuangalia mwanzo mwisho changamoto za hawa wafanyabiashara wakubwa , wa kati na wadogo changamoto nyingi ziko kwenye upande wa sera na muundo wa kitaasisi," amesema Bashungwa.

Aidha Bashungwa amemshukuru aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Joseph Kakunda kwa kusukuma gurudumu la Wizara hiyo tangu alipoteuliwa.

Awali, Bashungwa alikuwa ni Naibu Waziri wa Kilimo.