Waziri Mwakyembe aiombea michango Taifa Stars


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaomba watanzania kuichangia timu ya taifa 'Taifa Stars' ambayo ipo Misri kwa ajili ya michuano ya AFCON 2019.

Fedha zitakazopatikana ni kwa ajili ya kuendelea kuiwapa nguvu timu hiyo ambayo inaendelea na kambi huko Misri kujiandaa na michuano hiyo.

"Siku ya Alhamisi asubuhi tutakuwa na zoezi kubwa ambalo litaluwa LIVE kwenye mitandao na television mbalimbali na kwenye radio ambapo tutafanya uchangiaji wa Taifa Stars. Nawahakikishia kila shilingi itakayopatikana itakwenda kwa vijana wetu, wasishindwe kwa kuvunjika moyo." amesema.

Dkt. Mwakyembe amesema, fedha zitakazochangwa si kwa ajili ya kuipeleka timu Misri na kuirudisha, hatuhitaji kuwaweka kwenye hotel nzuri (hayo yote yameshafanyika) tunahitaji kufanya kitu ili timu yetu ifanye vizuri, motisha.