Loading...

7/14/2019

Alichosema Zacharia Hans Poppe kwenye Semina ya Simba SC hii leo


Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema malengo yao ni kutetea Ubingwa wa Ligi na kushinda ule wa bara Afrika.

Amesema hayo leo wakati akifunga semina elekezi kwa wachezaji wa kikosi hicho kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) wa mwaka 2019/20.

"Malengo yetu ya msimu ujao ni kutetea ubingwa wa Ligi Kuu na kushinda ubingwa wa Afrika ndio maana tumesajili wachezaji wenye viwango vikubwa, mjitume ili tufikie malengo" alisema Zacharia Hans Poppe.

Kwa upande wake Mulamu Nghambi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi alisema, "Tunataka kuwa moja ya timu tano bora Afrika, na kufika huko kuna mambo mengi yanahitajika kufanyika".

Loading...