Loading...

7/11/2019

Azam FC yamsajili mshambuliaji raia wa Ivory Coast

Klabu ya Azam FC imekamilisha taratibu za kumsajili kiungo mshambuliaji, Richard Djodi, kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa usajili huru akitokea kwa vigogo wa Ghana, Ashanti Gold.

Huo ni usajili wa mwisho kwa Azam FC kwa ajili ya msimu ujao, ikiwa hadi sasa imesajili wachezaji wapya watano, watatu wakiwa wa kigeni na wawili wazawa.

Djodi raia wa Ivory Coast, anayemudu kucheza nafasi zote za ushambuliaji, alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 17 na pasi 13 za mwisho, katika mechi 35 alizoichezea Ashanti Gold huku katika mechi 12 za mwisho akipiga manne.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Etienne Ndayiragije, ni Idd Seleman 'Nado', Selemani Ndikumana, Emmanuel Mvuyekure na Abalkasim Khamis.
Loading...