Balozi wa Afrika Kusini nchini aitaka jamii kuwawezesha Watoto wa kike kwenye Sayansi


Na Ferdinand Shayo-Arusha

Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku ameitaka jamii ya Watanzania kuwawezesha watoto wa kike katika masuala ya  teknolojia na sayansi ili waweze kuchochea maendeleo katika bara la Afrika kupitia sayansi na hata kupelekea maendeleo ya viwanda  nchini Tanzania na  barani Afrika  kwa ujumla.

Akizungumza katika ufunguzi wa Wiki ya Nelson Mandela inayofanyika katika Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela kilichopo jijini Arusha ambapo ameitaka jamii kuhamasisha na kujikita zaidi katika masomo ya sayansi ambayo yanachochea ugunduzi na uvumbuzi utakaosaidia maendeleo ya Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.

Kaimu Makamu wa Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela Profesa Antony Mshandete amesema kuwa katika maadhimishom ya siku ya kuzaliwa kwa nelson  Mandela wanatafakari jinsi ambavyo Ubunifu,Ugunduzi na Uhandisi unachangia kufikia uchumi wa viwanda na kuharakisha maendeleo kwa ujumla.

Kwa upande wao Mwanafunzi  wa Kike waliyefika katika Wiki ya Mandela Linda  Mathayo kutoka shule ya Star High Duluti amesema kuwa wiki hiyo imewapa hamasa ya kusoma masomo ya sayansi ili waweze kuwa Wahandisi,Marubani na Watafiti na pia kuondoa utamaduni potofu wa kuwa masomo hayo wanayaweza watoto wa kiume peke yao

Dr.Lilian Pasape ni Mhadhiri Mwandamizi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Mandela amesema kuwa katika wiki ya Mandela watakua na mafunzo Maalumu ya kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi pamoja kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wanaozunguka chuo hicho.