https://monetag.com/?ref_id=TTIb Chama cha Upinzani chashinda uchaguzi Ugiriki | Muungwana BLOG

Chama cha Upinzani chashinda uchaguzi Ugiriki


Kiongozi wa upinzani wa chama cha kihafidhina nchini Ugiriki Kyriakos Mitsotakis ameshinda uchaguzi wa bunge uliofanyika jana Jumapili ambao umetoa pigo kwa waziri mkuu Alexis Tsipras aliyeiongoza Ugiriki kwa miaka minne wakati wa mzozo mkubwa wa kifedha.

Chama cha New Democracy cha mwanasiasa Mitsotakis kimepata asilimia 39.8 ya kura ikilinganishwa na asilimia 31.5 za chama cha mrengo wa shoto cha Syriza cha waziri mkuu Tsipras. Mitsotakis ambaye atakuwa waziri mkuu ajaye, ameahidi kupunguza kiwango cha kodi, kuvutia uwekezaji na kubuni nafasi zaidi za kazi.

 Kwenye uchaguzi huo, chama cha mrengo mkali wa kulia cha Golden Dawn ambacho kiliundwa na wanazi mamboleo kimeshindwa kurejea bungeni katika matokeo yanayoashiria kupotea uungwaji mkono wa chama hicho kilichokuwa cha tatu kwa ukubwa katika bunge la Ugiriki.