Diwani wa Lindi bado asema CUF ipo imara na tishio kwa CCM



Na Ahmad Mmow, Lindi.

Licha ya chama cha CUF kuhamwa na wanachama wengi,baada ya aliyekuwa katibu mkuu wake, Seif Shariff Hamad kuhamia chama cha ACT-Wazalendo.

Diwani wa viti maalum wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Zainabu Lipalapi (CUF) amesema chama hicho kitaendelea kuwa imara na tishio kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lipalapi ameyasema hayo, leo alipozungumza na Muungwana Blog katika Manispaa ya Lindi. 3. Alisema  wimbi la kuhamwa na baadhi ya wanachama na viongozi haliwezi kudhoofisha wala kuuwa chama hicho ambacho kinauzoefu wa kupitia misukosuko inayosababishwa na migogoro.

Diwani huyo alisema hakiwezi kuyumba kwasababu ya kuhamwa na baadhi ya wanachama wakati kimepitia migogoro mikubwa na mizito na kiliweza kukabiliana nayo. '' CUF huwezi kukilinganisha na vyama vingine ambavyo havijakutana na misukosuko.Kitaendelea kuwa imara nakitakuwa tishio kwa chama tawala.

Kitawashangaza wengi, hasa ambao wanashindwa kukumbuka kimepitia magumu mangapi,'' alisema Lipalapi.

Kutokana na imani yake hiyo, alisema atakuwa wa mwisho kuhama chama hicho. Huku akibainisha kwamba hawezi kufanya hivyo kwani sasa ni taasisi inayoaminiwa na wananchi wengi.

Katika hali inayoonesha alijiapiza kutohama,  Lipalapi alikumbushia alikotokana nacho hadi sasa.

 Ambapo alisema walikuwa wanahutubia miti badala ya watu wakati chama hicho kikiwa kipya.

 '' Simkimbii mtu, kwani alikuta na anaweza kutuacha akahamia chama kingine. Watakaobaki nitakuwa nao, lakini CUF nisawa na mti wenye matunda matamu, lazima upigwe mawe,'' alisisitiza.

Hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama hicho wa wilaya ya Lindi, akiwamo mwenyekiti wa wilaya ambae pia alikuwa mbunge wa jimbo la Lindi (2010-2015), Salum Barwany walikihama chama hicho na kujiunga na vyama vingine.