Fahamu athari za minyoo katika ufugaji wa kuku


Ufugaji wa kuku una changamoto lukuki, miongoni mwa changamoto hiyo ni pamoja na kuku kupatwa magonjwa. Siku ya leo naomba nikualike rasmi jamvini ili tuweze kuangazia akili na macho yetu katika suala la minyoo.

Minyoo kwa kuku ina athari nyingi, athari ambazo zinaweza kumpata  hasara kubwa mfugaji wa kuku kama hatozingatia ratiba ya kuwapa dawa ya minyoo kuku wake kila baada ya miezi mitatu.

Athari za minyoo kwa kuku ni kama zifuatazo:-
Minyoo mara zote ndani ya mwili wa kuku hutumia virutubisho vyote ambavyo tayari vishameng'enywa na kuku, hali ambayo humfanya kuku kushindwa kurudisha au kufidia nguvu (digestible energy)  aliyoipoteza katika kumeng'enya chakula.

Pia athari nyinbgine ya minyoo ni kwamba kuku  atashindwa pia kupata virutubisho vya ukuaji (nutrients  for growth).

Kama hiyo haitoshi  pia kuku atakosa kupata virutubisho vya uzalishaji (nutrients for production), hali ambayo itamfanya kuku kudhoofika, kudumaa, kupunguza au kutotaga kabisa na hatimaye kufa.

Kumbuka; Ewe mfugaji unashauriwa ya kwamba kuwapa kuku wako dawa wa kutibu minyoo kila baada ya miezi mitatu.