https://monetag.com/?ref_id=TTIb Haya ndio maneno ya Bashe kwa Rais Magufuli | Muungwana BLOG

Haya ndio maneno ya Bashe kwa Rais Magufuli


Naibu waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake majukumu aliyopewa kusukuma gurudumu la maendeleo.

Bashe ametoa kauli hiyo leo wakati wa hafla ya kuapishwa kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam, huku akisema Sekta ya kilimo ina changamoto na anaahidi kuzishughulikia.

"Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kwa yale niliyopewa ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele, Sekta ya kilimo ina changamoto na ninaahidi kuzishughulikia, sitokuangusha na nitatimiza wajibu wangu,” amesema Bashe.

"Mh. Rais nakushukuru kwa imani yako juu yangu na Wananchi wa Nzega, nalifahamu sana suala la Kilimo nafahamu changamoto hizi ambazo zimeajiri 70% ya Watanzania nilizoea kuzisikia tu sasa ntazipata field."

Bashe ambaye ni Mbunge wa Nzega aliteuliwa jana na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.