Loading...

7/14/2019

Kenya yatoa wito wa kushirikiana kupambana na ugaidi baada ya shambulizi la Somalia


Hapo jana nchi ya Kenya ilitoa wito kwa dunia kuungana kwenye mapambano dhidi ya ugaidi baada ya kundi la wanamgambo wa Somalia al-Shabaab kuua watu 26, miongoni mwao wakiwemo Wakenya watatu, kusini mwa Somalia.

Akitoa salamu za rambi rambi kwa familia na marafiki wa watu waliopoteza maisha yao, waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Monica Juma, ameitaka jumuiya ya kimaifa kuharakisha kuliorodhesha kundi la al-Shabaab kama shirika la kigaidi chini ya azimio namba 1267 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili kusaidia kukabiliana na washirika hao wa kundi la kigaidi la al-Qaida.

Mkuu wa Jimbo la Jubbaland Ahmed Mohamed Madobe, amesema wageni 10 kutoka Kenya, Canada, Marekani na Tanzania ni miongoni mwa waliouawa baada ya gari lililojazwa mabomu kuvamia hoteli ya Medina mji wa Kismayo, kabla ya washambuliaji kuingia ndani ya hoteli na kujilipua.
Loading...