LIVE: Rais Magufuli akiwaapisha George Simbachawene na Hussein Bashe


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mhe. George Boniface Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. January Yusuf Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amuapisha Bw. Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo. Mhe. Bashe anachukua nafasi ya Mhe. Innocent Lugha Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.