Liverpool yakataa kumuachia Divock Origi

Msha,mbuliaji wa klabu ya Liverpool Divock Origi amesaini mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo baada ya kuonyesha kiwango cha kuridhisha msimu uliopita.

Origi ambaye ni raia wa Ubelgiji alikua amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake uliosalia aliweza kufunga magoli mawili kwenye mchezo wa nusu fainali ambayo Liverpool iliifunga Barcelona 4-0.