Maelfu waandamana kufuatia kesi ya ubakaji ya mtoto wa miaka miwili

Maelfu ya watu wamemiminika barabarani mjini Yangon wakati hasira zikipanda kuhusiana na kubakwa kwa mtoto wa miaka miwili, kufuatia kampeni iliyosambaa mitandaoni kuwataka watu wa Mnyanmar kuandamana.

Kisa hicho kilitokea mwezi Mei katika mji mkuu wa Mnyanmar Naypyidaw lakini kampeni ya Ummah ilipamba moto wili iliyopita baada ya babake mtoto kuzungumza na vyombo vya habari nchini humo akikasiriswa na hatua ya namna uchunguzi juu ya kisa hicho unavyoendeshwa.

 Waandamanaji waliandamana hadi katika idara ya upepelezi wa uhalifu Kaskazini mwa mji huo, wengi wakivalia nguo nyeupe na kubeba mabango yaliyoandikwa tunataka haki kwa mtoto huyo wa kike pamoja na usalama bora kwa watoto wa taifa hilo.

Mwanamume mmoja alikamatwa siku ya Jumatano nakushtakiwa kwa kosa hilo la ubakaji lakini wakaazi wanawasiwasi iwapo serikali imempata mtuhumiwa wa kweli au la.