Maneno ya Rais Magufuli kwa Bashe 'nakusikilizaga sana Bungeni michango yako'


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa anamsikilizaga sana Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo kwasasa.

Rais Magufuli amesema kuwa michango ya Mbunge huyo ni mizuri anatoa uchambuzi na umemvutia sana hivyo ametaka zile za Bungeni sasa aziweke kwenye utekelezaji.

"Nakusikilizaga sana bungeni, michango yako ni mizuri, unatoa analysis na zimenivutia, zile zilikuwa za bungeni sasa ziwe kwenye utekelezaji, na ukatekeleze kwelikweli," amesema Rais Magufuli katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliwateua jana.

 Hata hivyo, Bashe alimuahidi Rais Magufuli kuwa hatomuangusha kwenye Wizara ya Kilimo.