Mauro Icardi kuondoka katika kambi ya Inter Milan


Mshambuliaji Mauro Icardi hatosafiri na klabu ya Inter Milan kwenda Asia baada ya kuondoka kambini kwa makubaliano yake na timu hiyo.

Jana Jumamosi klabu ya Inter kupitia mtandao wao wa twita walitoa taarifa ya mshambuliaji huyo kurejea Milan akitokea katika kambi ya timu hiyo Switzerland na hivyo hatakuwa na kikosi chao kinachoenda Asia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Mshambuliaji huyo wa Argentina hayupo katika mipango ya kocha mpya wa Inter Milan Antoine Conte, ikiripotiwa kuwa anatarajiwa kuuzwa.

Icardi,26, ambaye alivuliwa unahodha wa Inter Milan msimu jana, anahusishwa kutakwa na Juventus, huku klabu za Man United na Napoli pia zikimmendea.