Loading...

7/14/2019

Messi aongoza kwa wanasoka wanaochukua mkwanja mkubwa


Lionel Messi staa wa timu ya Taifa ya Argentina anayekipiga kwenye klabu ya Barcelona ni miongoni mwa nyota wanaoingiza mkwanja mrefu kutokana na kipaji chake.

Anakuja kiasi cha pauni milioni 7.5 kwa mwezi sawa na sh.bilioni 21.5 za kibongobongo.

Ndiye staa anayeongoza kwa kukunja mkwanja mrefu duniani kwa wanasoka wote ngoma inakwenda mpaka mwaka 2021 ni kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Amepachika jumla ya mabao 614 katika mechi 719 tangu aanze soka la kulipwa mwaka 2004 huku mpinzani wake Cristiano Ronaldo anayekipa Juventus akipokea mshahara wa pauni milioni nne sawa na bilioni 11.4 za kibongobongo.
Loading...