Mvua kubwa zaua watu nchini China


Watu watatu wamefariki na wengine 23 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko katika mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China.

Mvua hiyo ilianza kunyesha siku ya Jumapili mwendo wa saa tatu usiku na kuathiri kundi la wataliii 285 walikokuwa wanazuru mlima wa Gaohu mjini Yichun.

Hadi kufikia sasa serikali ya nchi hiyo imewatuma waokoaji zaidi ya 530 katika eneo hilo kwa shughuli ya kuwaokoa majereh na kutoa misaada zaidi.