Loading...

7/11/2019

Mwanamuziki Nicki Minaj afuta tamasha lake la Saudia

Nicki Minaj, mwanamuziki kutoka Marekani amehairisha tamasha alilokuwa alifanye Saudia ambalo lengo lake lilikuwa kutetea haki za wanawake.

Nicki Minaj alisema baada ya kufikiria kwa muda mrefu amechukua uamuzi wa kuahirisha kutumbuiza katika tamasha la dunia la Jidda.

Tamasha hilo lilipangwa kufanyika tarehe 18 Julai mjini Jidda katika uwanja wa mfalme Abdullah. Pamoja na waandaaji wa tamasha hilo nchini Saudia kutangaza kwamba tamasha hilo lingesambazwa dunia nzima na wote ambao wangetaka kuhudhuria wangepatiwa urahisi wa kupata viza kwa njia ya kimtandao, tamasha hilo lilidhua upinzani mkubwa ndani nan je ya nchi hio.

Tangu kuteuliwa kuwa mwanamfalme mrithi wa kiti cha enzi, Muhammed bin Salman mtoto wa mfalme Salman amechochea mabadiliko ya aina mbalimbali nchini huo. Tamasha la muziki la Jidda ni katika mabadiliko hayo, Ni kwa mara ya kwanza tamasha hilo linafanyika nchini Saudia.
Loading...