Rais Magufuli kukutana uso kwa uso na wafugaji wote Tanzania


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa amepanga siku za hivi karibuni kukutana na Wafugaji wote Tanzania kama alivyozungumza na watu wa Madini, wafanyabiashara.

Rais Magufuli amesema hawezi kupotozea changamoto za wafugaji hasa katika kushughulikia maeneo ya kuchungia mifugo yao.

"Nimepanga siku za usoni nitakutana na wafugaji wote wa Tanzania, kama tulivyozungumza na watu wa madini, kama ambavyo tulizungumza na Wafanyabiashara, hatuwezi kuignore changamoto zao hasa katika kushughulikia maeneo ya kuchungia mifugo yao," amesema Rais Magufuli leo Ikulu katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni.

"Ng'ombe tunao wengie, mpaka sasa tuna Ng'ombe zaidi ya Million 5.5, nitakaa na wafugaji niwasikilize watoe ushauri wao ili tuweze kuwasaidia wafugaji wa Watanzania ili ufugaji uweze kuleta impact ya uchumi wa nchi yetu."