https://monetag.com/?ref_id=TTIb RC Dodoma.Dkt.Mahenge ahimiza wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa | Muungwana BLOG

RC Dodoma.Dkt.Mahenge ahimiza wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa



Na.Enock Magali,Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt,Binilith mahenge,amewasihi wananchi  kuhakikisha wanajiunga na Bima ya Afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa ili iweze kuwasaidia na kuwarahisishia gharama za matibabu pindi wanapokwenda kupata huduma za Afya.

Dkt.Mahenge ameyasema hayo,wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa katika kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa Wilayani Chamwino,ambapo amesisitiza kuwa hata anapokwenda kwenye mikutano wananchi watakaopoewa kipaumbele cha kusikilizwa changamoto zao kwenye sekta ya afya ni wale tu wenye kadi za CHF.

"Na mimi Mkuu wa Mkoa,nikija kwenye Mkutano mwananchi unataka kutoa shida kwenye sekta ya Afya,jambo la kwanza nitakwambia nioneshe kama una kadi ya CHF, ndio tuendelee kuskilizana"Dkt.Mahenge.

Aidha pia amewataka viongozi katika ngazi zote,kuhakikisha zoezi hilo linakuwa la kudumu  ambapo ameziagiza wilaya zote ndani ya mkoa wa Dodoma,kuhakikisha zinawasilisha taarifa za wananchama walioandikishwa katika Bima hiyo kwa katibu Tawala wa Mkoa kila mwezi.

"Katibu Tawala Mkoa kwa kuwa upo hapa, hii ni pamoja na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma  na Wakurugenzi wa Halmashauri zote, lazma tuhakikishe kaya zote 447,773 Dodoma zinajiunga na CHF iliyoboreshwa ifikapo Disemba 2019,ili kweli tufanikiwe katika hili ni lazima tufanye operation kama ile tuliyoifanya kwenye vitambulisho vya Wajasiriamali na kama tulivyofanya katika kampeni ya kusajili vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5"Dkt Mahenge.

"Mganga Mkuu wa Mkoa na Waganga wakuu wa Wilaya,hakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma bora kwa wanachama wa CHF kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ili waweze kutoa ushuhuda mzuri kwa wananchi ambao hawajajiunga na CHF"Aliongeza.

Akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa CHF,Mratibu wa CHF Mkoa wa Dodoma,Dr.Francis Lutalala yeye amesema kuwa katika mikoa 22 inayotekeleza mpango wa CHF kuanzia mwezi July 2018 mpango ulipoanza kutekelezwa kitaifa mkoa wa Dodoma umeendelea kuwa kinara na kuongoza kwa kaya elfu 17 kwa usajili wa wanachama.

"Hadi kufikia tarehe 22 Novemba,2018 wakati wa uzinduzi rasmi wa CHF iliyoboreshwa kule wilayani Mpwapwa, jumla ya kaya zilizokuwa zimejiunga na CHF kwa kitita cha shilingi 30,000 zilikuwa ni kaya 1,467 Kufuatia utekelezaji wa maelekezo yako wakati wa uzinduzi, hatua mbalimbali zimetekelezwa kuhakikisha wananchi wengine zaidi wanajiunga, na hivyo hadi kufikia tarehe 30 ya mwezi Juni,2019 Mkoa umeandikisha jumla ya kaya 17,366."Dr.Lutalala.

"Takwimu za kitaifa zinaonesha kati ya Mikoa 22 inayotekeleza mpango wa CHF iliyoboreshwa kuanzia Julai 2018 mpango ulipoanza kutekelezwa, Mkoa wa Dodoma umeendelea kuwa kinara na kuongoza kwenye usajili wa wanachama wa CHF (kaya 17,366) na makusanyo ya Shilingi 520, 980,000/- mpaka kufikia tarehe 30 Juni, 2019"Aliongeza.

Nao baadhi ya wananchi waliozungumza na Blog hii wamekiri kutumia gharama kubwa pindi wanapokwenda kutibiwa pasi na Bima na kusema kuwa elimu waliyopewa imewafungua na kuahidi kukata bima hizo.