Urusi yazindua darubini itakayotumika kupima nishati ya joto angani


Nchi ya Urusi imezindua darubini ya Spektr-RG itakayotumika kwa kupima nishati ya joto angani. Darubini hiyo inatarajiwa pia kutambua idadi mpya ya vyanzo vya nishati, kama vile mashimo makubwa meusi yaliyopo katikati mwa nyota nyingi.

Darubini hiyo itasafiri katika eneo linalochunguzwa zaidi yapata kilomita milioni 1.5 kutoka duniani linalofahamika kama -Lagrange Point 2.

Spektr-RG kimetengenezwa kwa muundo wa darubini mbili kwa pamoja kwa ushirikiano na Ujerumani.