Wafa maji wakikwepa kushambuliwa na Viboko Ziwa Babati


Na John Walter, Babati

Watu wawili wamepoteza maisha wakati wakiwa kwenye shughuli zao za uvuvi wa samaki  Ziwa Babati mkoani Manyara usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa miili ya watu hao Paulo Elias(45)  na Nicomed Peter (43) wote wakazi wa mtaa wa Nangara mjini Babati,walikutwa wakiwa  pembezoni mwa ziwa hilo huku mitumbwi waliyokuwa wakiitumia ikielea juu ya maji.

Kamanda Senga ameeleza kwamba miili hiyo ipo hospitali ya mji wa Babati Mrara kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Ziwa hilo linakisiwa kuwa na viboko wengi ambao wanahatarisha maisha ya wakazi wanaozunguka ziwa hilo pamoja  na wavuvi kwani ndani ya siku mbili pekee tayari watu watatu wamepoteza maisha wakijihami na Viboko hao