Loading...

7/11/2019

Waziri mkuu wa Israel Netanyahu aitolea vitisho Iran

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema ndege za kivita F-35 ilizonazo Israel zinaweza kufika Iran ukijumuisha na Syria na kila kona ya mashariki ya kati.

Netanyahu alitoa vitisho kwa Iran alipozuru kambi ya jeshi la anga ya Nevatim  iliyopo kusini mwa nchi hiyo.

Netanyahu alisema kwamba siku za hivi karibuni Iran imekuwa ikitishia kuifuta Israel katika uso wa dunia akaongeza kwamba nataka awakumbushe kwamba ndege vita F-35  walizonazo zinaweza fika Iran ukijumisha na Syria pamoja na kila kona ya mashariki ya kati.

Netanyahu ambaye mara kwa mara huishutumu Iran kwa kuwa na lengo la kutengeneza silaha za nyuklia alimalizia kwa kusema kwamba hata kama Israel itabaki peke yake haitaruhusu Iran iwe na silaha za nyuklia kamwe.
Loading...