Loading...

8/11/2019

Azam FC waanza vibaya Kombe la Shirikisho Afrika


Timu ya Azam FC imeanza kwa kuchechemea kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema baada ya kukubali kichapo cha 1-0.

Mchezo huo umechezwa uwanja wa Bahir, Dar, nchini Ethiopia na bao la ushindi lilipatikana kipindi cha kwanza dakika ya 45 kupitia kwa Bezabeth Meleyo.

Jitihada za wachezaji wa Azam FC kupata bao la kusawazisha kipindi cha pili ziligonga mwamba na kufanya mpaka dakika 90 kukamilika wakiwa nyuma kwa bao 1. Mchezo wa marudio utachezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Chamanzi na Azam FC.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger