Bangladesh: Watu 25,000 wagunduliwa kuugua ugonjwa wa Dengue


Watu 25,000 wamegunduliwa kuugua ugonjwa wa homa wa Dengue nchini Bangladesh huku 18 wakiaga dunia.

Mkurugenzi wa Taasisi ya serikali ya Epidemologia, udhibiti wa magonjwa na utafiti (IEDCR), Mirjadi Mehjabin, ameelekeza mikoa na halmashauri zote nchini kuweka jitihada za udhibiti kwa kunyunyizia dawa ya viuadudu kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu waenenezao ugonjwa huo.