https://monetag.com/?ref_id=TTIb Cristiano Ronaldo akiri kuteswa na tuhuma za ubakaji | Muungwana BLOG

Cristiano Ronaldo akiri kuteswa na tuhuma za ubakaji


Mchezaji Cristiano Ronaldo alikuwa na tuhuma za ubakaji, kosa ambalo anadaiwa kulitenda miaka 10 iliyopita katika mji wa Las Vegas Marekani.

Tuhuma hizo zilifutiliwa mbali hivi karibuni baada ya mlalamikaji kushindwa kutoa uthibitisho wa kutosha kuhusiana na kesi hiyo.

Ronaldo akihojiwa na kituo cha TV1 cha kwao Ureno ametaja tuhuma hizo ziilimfanya aone mwaka 2018 ndio mwaka mbaya katika maisha yake.

"Mwaka 2018 inawezekana ndio ukawa mwaka mbaya zaidi katika maisha yangu, binafsi nazungumza. Wakati mtu anakuwa ana swali juu ya heshima yako inaumiza, inaumiza sana" alisema Ronaldo

“Inaumiza vikubwa kwa sababu nina familia kubwa, mke na mtoto mwerevu ambaye anaweza kuelewa vitu vingi. Hili suala sipo vizuri kulielezea. Lakini kwa mara nyingine tena, nimethibitika sina hatia, imenifanya nijisikie fahari.”

Hata hivyo Ronaldo hakutaka kuzungumzia moja kwa moja tuhuma hizo zilizodaiwa kutokea mwaka 2009 kwa kudaiwa kumbaka mwanadada huyo Kathryn Mayorga ambaye awali ilitajwa kuwa alipewa dola 375000 ili kusaini makubaliano ya kukaa kimya kuhusiana na suala hilo.