Inter Milan watua Uingereza kumnyakua Alexis Sanchez

Wawakilishi wa klabu ya Inter Milan wapo nchini Uingereza kwaajili ya kufanya mazungumzo na klabu ya Manchester United juu ya kumsajili Alexis Sanchez.

Sanchez anakaribia kwenda klabu hiyo inayoshiriki Serie A, wapo katika kukubaliana na United kuhusu ada ya mchezaji huyo mwenye miaka 30 raia wa Chile.