https://monetag.com/?ref_id=TTIb Israel: Waumini wa dini ya kiislamu wakabiliana vikali na Polisi | Muungwana BLOG

Israel: Waumini wa dini ya kiislamu wakabiliana vikali na Polisi


Waumini wa dini ya kiislamu wamekabiliana vikali na Polisi Israel katika eneo takatifu la msikiti wa Al Aqsa mjini Jerusalem mapema leo wakati wa dua za kuadhimisha sikukuu ya Eid el Hajj.

Takribani wapalestina 14 wamejeruhiwa kwenye makabiliano hayo na mmoja wao yumo kwenye hali mahututi.

Kisa hicho kimetokea siku moja baada ya wanajeshi wa Israel kuwaua walinda usalama 4 wa Palestina ambao wanadaiwa kuwa walijaribu kufanya mashambulio katika eneo la mpakani.