Kiswahili sasa rasmi ndani ya SADC


Wakuu wa nchi wa SADC wameipitisha lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya nne itakayotumika katika shughuli rasmi za jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa SADC ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametangaza rasmi leo uamuzi huo baada ya kukabidhiwa kijiti hicho hapo jana.

Muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa SADC Rais Magufuli kutangaza kupitishwa kwa Kiswahili kuwa lugha ya nne katika shughuli za SADC, Rais wa Msumbuji, Filipe Nyusi alipoongea kwa Kiswahili katika hotuba yake ya kutoa shukrani.

Katika hatua nyingine kuhusu nchi ya Zimbabwe kuwekewa vikwazo mbalimbali, Rais Magufuli amesema kuwa wamekubaliana kuwa wataendelee kufanya mawasiliano na jumuiya za kimataifa ili kuwezesha kuondolewa kwa vikwazo kwenye nchi hiyo.