Loading...

8/19/2019

Lori la Mafuta lapinduka na kuwaka moto Uganda


Watu zaidi ya 10 wamekufa na wengine kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto eneo la kibiashara Kyambura wilayani Kibirizi nchini Uganda.

Mkuu wa Wilaya ya Rubirizi, Harriet Nabukenya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo hapo jana na kusema dereva wa lori la mafuta alishindwa kudhibiti mwendo wa lori hilo na kuvamia teksi mbili za abiria zilizokuwa zimeegeshwa barabarani.

Baada ya sekunde kadhaa lori hilo liliwaka moto ambao ulienea katika nyumba na maduka kadhaa na kuteketeza vitu. Wazima moto ambao walifika katika eneo hilo saa moja baada ya tukio, wameokoa baadhi ya mali.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger