https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mabalozi 5 wa nchi za Africa mashariki waudhuria ufunguzi wa wiki ya uwekezaji Kagera | Muungwana BLOG

Mabalozi 5 wa nchi za Africa mashariki waudhuria ufunguzi wa wiki ya uwekezaji Kagera

Mabalozi wa chi tano za Africa mashariki na kati wameudhuria ufunguzi wa wiki ya uwekezaji Kagera ili kujionea fursa zinazopatikana mkoani Kagera na kuwaelezea wawekezaji na wafanyabiashara fursa zilizopo nchini mwao.

Awali akitoa salamu za mkoa Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jeneral Elisha Marco Gaguti amesema kuwa wageni wote waliotoka waliokuja watapata nafasi ya kutembelea maeneo ya uwekezaji yanayopatikana mkoani Kagera ambapo itakuwa itasaidia kukuza uwekezaji wa mkoa na taifa ujumla.

Wiki ya uwekezaji Kagera imeanza leo Agosti 12/2019 ambapo inatarajiwa kumalizika Agosti 17 mwaka huu. Wafanyabiashara mbali mbali kutoka Nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC Congo.

Katika mkutano wa mkuu wa mkoa Kagera na wafanyabiashara, wawekezaji na mabalozi wa nchi za Africa mashariki unaoendelea katika ukumbi wa ELCT BUKOBA mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jeneral Marco Elisha Gaguti na wajumbe wa kikao hicho wametumia dakika moja kuwakumbuka marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya moto huko mkoani Morogoro.