Maelfu washiriki kwenye maandamano Hong Kong

Maelfu ya wafuasi wa wanaharakati wanaotetea demokrasia mjini Hong Kong wakiwemo walimu, leo hii Jumamosi wamejitokeza katika maandamano ya kupinga serikali licha ya kwamba mvua kubwa inanyesha.

Hata hivyo kuna hofu kwamba polisi wanaweza kutumia nguvu katika kuwatawanya waandamanaji hao.

Kufuatia kuongezeka kwa vurugu katika siku zilizopita, maandamano wikiendi hii ni kama mtihani kwa wanaharakati hao kuonesha kama harakati hiyo bado inaungwa mkono na watu wengi.

Wakati huo huo huko mjini Sydney, Australia idadi kubwa ya waandamanaji wanoiunga mkono China, wameandamana kama ishara ya kujibu wanaounga mkono maandamano ya demokrasia ya mjini Hong Kong.

Waandamanaji hao walipeperusha bendera za China huku wakiimba "China moja". Mivutano kati ya makundi hayo mawili inazidi kuongezeka huko nchini Australia.