https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mbunge aipiga jeki shule ya sekondari Kililima | Muungwana BLOG

Mbunge aipiga jeki shule ya sekondari Kililima


Na. Ahmad Mmow, Kilwa

Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya elimu. Mbunge wa jimbo la Kilwa Kasikazini, Veda Ngombale amekabidhi mifuko 50 ya saruji kwa shule ya sekondari ya kata ya Mingumbi inayotambulika kwa jina la  Kililima.

Akizungumza na wananchi katika kijiji cha Kililima, baada ya kukabidhi saruji hiyo yenye thamani ya shilingi 750,000,  Ngombale alisema wananchi hawanabudi kujitolea na kuchangia shughuli na ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao.

Ngombale aliweka wazi kwamba yeye kama mbunge anakila sababu ya kuunga mkono juhudi za wananchi na kushirikiana nao kutatua changamoto na kero zinazowakabili.

Alisema pamoja na wajibu wake wa kuwasemea, kuwaunga mkono juhudi zao na serikali. Lakini wasiache kutimiza wajibu wao wa kujitolea nguvu na mali kuchangia  ujenzi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na iliyopo katika vijiji vyao.

''Niwajibu wangu kama mbunge kushirikiana na wananchi, nimekabidhi bomba za kupandisha maji kutoka pango la Nang'oma ili kupunguza tatizo la maji katika kijiji cha Nandembo. Wakati serikali ikiwa kwenye mkakati wa kuondoa tatizo la maji katika vijiji vyenye tatizo hilo. Ikiwamo Nahama, muda si mrefu kazi ya kuchimba visima itaanza,'' alihaidi Ngombale.

Aidha Ngombale aliwatoa hofu wananchi ambao ujenzi wa zahanati za vijiji vyao umesimama, alisema '' Kuhusu ujenzi wa zahanati ambazo ujenzi wake umesimama kama ile ya Nambondo, Kandawale, Nahama na nyingine. Tayari zipokwenye mpango, kwasasa vimeanza vikao vya maandalizi ya kikao cha baraza. Baada ya kumalizika kikao cha baraza kuna uwezekano mkubwa mipango itakuwa imekamilika na ujenzi wa zahanati hizo utaanza,'' aliahidi tena na kuwapa matumaini wananchi.

Mifuko hiyo ya saruji iliyotolewa kwa shule ya sekondari Kililima inatarajiwa kutumika kwa ukarabati wa majengo ya shule hiyo.