Muigizaji The Rock afunga ndoa na Lauren Hashian


Muigizaji Dwayne Johnson maarufu kama The Rock amefunga ndoa na muimbaji Lauren Hashian kando ya fukwe za Hawaii. Johnson, 47, na Hashian, 34, ni wazazi wa mabinti wawili Jasmine, 3, na Tiana, 1.

Utakumbuka kuwa kabla ya ndoa hiyo, Johnson alibahatika kupata mtoto pia kwenye mahusiano yake yaliyopita na bibie Dany Garcia.

Wawili hawa wanatajwa kukutana mwaka 2006 na kuanza rasmi mahusiano ya kimapenzi mwaka 2007 baada ya ndoa ya The Rock Dany Garcia kuvunjika.