Loading...

8/06/2019

Mwendesha baiskeli afariki akiwa kwenye mashindano


Mwendesha baiskeli wa Ubelgiji Bjorg Lambrecht amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 22 baada ya kupata ajali akiwa kwenye hatua ya tatu ya Tour de Pologne.

Ajali ya Lambrecht ilitokea umbali wa maili 60 kufikia mwisho wa mbio hizo zilianzia Chorzow na kuishia Zabrze nchi Poland.

Alikimbizwa hospitali kwa helikopta ambako baadaye alifariki. Lambrecht amefariki wakati akifanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha makali.

Mkurugenzi wa mbio Czeslaw Lang amesema eneo alilopata ajali halikuwa na mtereko hadi kufanya akimbie kwa kasi, bali ilikuwa barabara pana iliyonyooka. Amesema alipata majeraha makubwa hadi waliita gari la wagonjwa na helikopta.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger