Ndege yasafirishwa kwa kubebwa na Helikopta hadi Uingereza


Ndege ya kijeshi inayomilikiwa na jeshi la anga la kifalme (RAF) yasafirishwa na ndege nyingine ya helikopta aina ya Chinook kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye makavazi nchini Uingereza.

Ndege hiyo maarufu kwa jina la The Hawk ilisafirishwa ikiwa imebebwa na helikopta kutoka kambi ya kijeshi ya Boscombe Down hadi makao yake mapya ya Sarum Airfield, karibu na Salisbury. Usafiri wa ndege hiyo iliyostaafishwa ulivutia wengi waliokuwa wakisafiri kati ya Salisbury na Amesbury.

Ndege hiyo ilikuwa inaninginia chini ya helikopta ya Chinook ikiwa imefungwa na kamba. (Picha/ Hisani ya Wizara ya Ulinzi-Unigereza).