https://monetag.com/?ref_id=TTIb Rais wa DR Congo atangaza Baraza jipya la Mawaziri | Muungwana BLOG

Rais wa DR Congo atangaza Baraza jipya la Mawaziri


Rais wa DR Congo, Felix Tsisekedi ametangaza baraza jipya la mawaziri.Baraza hilo limetangazwa hii leo baada ya kusubiriwa kwa miezi Saba.

Katika serkali hiyo mpya, wanawake wamepewa asilimia 17 ya mawaziri na wanaume ni asilimia 83. Pia imeundwa wizara maalum ambayo itashughulikia masuala ya watu wenye ulemavu.

Ikumbukwe July  mwaka huu Rais Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda serikali ya muungano itakayokuwa na mawaziri 66.

Katika makubaliano yao chama cha rais huyo wa zamani sasa kimepata wizara 43, na kile cha rais Félix Tshisekedi kimechukua wizara 23.