Loading...

8/12/2019

RC Moro azungumzia hali za majeruhi

Majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea juzi Jumamosi Agosti 10,2019 mkoani Morogoro nchini Tanzania inaendelea vyema huku miili 60 imezikwa jana Jumapili katika makaburi ya kola Mkoa huo.

Hadi jana jioni, vifo vilivyokuwa vimeripotiwa kutokana na ajali hiyo ni 72 na majeruhi zaidi ya 59 ambapo baadhi wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na wengine wakihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi,

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Agosti 12,2019 akiwa katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro.

Dk Kebwe amesema majeruhi 16 waliopo hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro na majeruhi 43 waliopo hospitali ya taifa ya Muhimbili inaendelea vizuri.

Amesema mpaka leo Jumatatu asubuhi familia mbili zimejitokeza kuzika marehemu wao wenyewe huku mwili mmoja ukipelekwa Sengerema mkoani Mwanza na Songea Mkoa wa Ruvuma.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger