Roketi ya biashara ya China yafanya safari ya kwanza


Roketi mpya ya kubebea mizigo ya China Smart Dragon-1, iliyotengenezwa kwa ajili ya matumizi ya biashara, imefanya safari yake ya kwanza leo, na kupeleka satalaiti tatu kwenye obiti.

Roketi hiyo iliyoendelezwa na kampuni ya roketi ya China, inayohusiana na Akademia ya Teknolojia ya kurusha Vyombo ya China CALVT, imeruka saa 6:11 mchana kutoka kwenye kituo cha kurushia satalaiti cha Jiuquan kilichopo Kaskazini Mashariki mwa China.

Satalaiti hizo tatu zitatumika kutoa huduma ya kuhisi kwa mbali, mawasiliano na internet kwa vitu. Mkuu wa CALVT Wang Xiaojun amesema, tofauti na roketi ya Long March family, roketi hiyo mpya ya Dragom imeendelezwa katika hali ya kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la kurusha satalaiti ndogo za biashara.