Sababu za Polisi kuwashikilia wanachama wa ACT-Wazalendo, Mwandishi hizi hapa


Tuhuma za kufanya maandamano bila kibali Wanachana watatu na mwandishi wa habari, Jeshi la Polisi wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Tanzania limesema linawashikilia.

Jumamosi hii  Jeshi la Polisi walizuia mkutano wa ndani wa chama hicho uliokuwa ufanyike katika wilayani hiyo.

Waliokamatwa ni Mwenyekiti wa jimbo la Ilala, Mwikizu Mayama; mwenyekiti wa chama hicho Temeke, Said Mohammed, Katibu wa uadilifu, Mbarala Maharagande na mwandishi wa habari wa televisheni mtandao ya Gillybon, Haruna Mpaunda.

Kamanda wa Polisi wilayani humo, Amoni Kakwale amesema waliokamatwa walikuwa wakiongoza maandamano bila kuwa na kibali.

"Kama unataka taarifa zaidi unaweza kufika ofisini mimi nakupa taarifa kama msemaji,  waliokamatwa walikuwa wakifanya maandamano kinyume na sheria,” amesema Kakwale.

Aidha amesema sababu za kukamatwa kwa mwandishi wa habari amesema hawezi kutofautisha mwandishi na mwanachama, wote wanahojiwa kwa kosa moja.