Shamsa Ford awatolea uvivu mashabiki zake


Ikiwa tayari ni miezi kadhaa imepita tangu Staa wa filamu nchini, Shamsa Ford kuachana rasmi na aliyekuwa mume wake, Chiddi Mapenzi, mapema wiki hii ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwakata ngebe wale aliowaita madoctor insta.

Shamsa amedai kuwa kwa sasa yupo 'busy' na biashara zake na hana 'stress' zozote zinazomsumbua.

Staa huyo ameamua kufanya hivyo baada ya kuwepo na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii yakimuhukumu kuwa ana mawazo kutokana na ishu nzima ya kuachana na aliyekuwa mume wake.

Hata hivyo, Shamsa alienda mbali na kusema kuwa alifanya maamuzi hayo kutokana na moyo wake pamoja na akili kuridhika na ana furaha kubwa kwa sasa.

Shamsa aliandika hivi;

Naomba niwachane nyie wote mnaojifanya madoctor humu insta..Hivi mm ndo wa kwanza kutoka kwenye ndoa?kwahiyo baada ya kutoka kwenye ndoa mlitegemea niwe mkiwa?nisicheze,nisifurahi hata nikicheka kwa kuonesha meno eti nina stress za kuachwa..Naomba mjue kitu kimoja am very happy with my life kwa sasa hivi sina stress hata moja zaidi ya kufikilia maisha,sanaa yangu na biashara yangu. Mpaka nikaamua kutoka basi moyo wangu na akili yangu ililizika.Mimi siyo mwanamke ninayeweza pigana na moyo wangu kama mtu nampenda nitampigania hata iweje coz siwezi kusema HAPANA mdomoni wakati moyoni mwangu kuna NDIYO.Kwahiyo mnikomee nyie madoctor wa vichocholoni kusema mm nina stess.chochote nachofanya basi ni maamuzi yangu na ninafurahia.IAM VERY HAPPY life is too short kuangalia ya kwangu badala ya kuangalia ya kwako