TAWESO yawafunda wakulima Misungwi

Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imewataka  wakulima kuhakikisha wanatumia kilimo cha kisasa ili waweze kupata mazao bora kwajili ya mazao ya biashara na chakula.

Akizungumza wakati kongamano la maonyesho ya biashara katika uwanja wa Mwanakanenge, Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Misungwi Diana Kuboja alisema ni wakati sasa wakulima kulima kwa tija ili waweze kunufanika zaidi.

Kuboja aliipongeza shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali kwa la ‘Global communities’ kwa kuleta maonyesho hayo ya wakulima wilayani hapa.

Aliwaomba wakurugenzi mbalimbali nchini kuhakikisha wanawaelekeza maafisa ugani wawe karibu zaidi na wakulima ili wakulima wawe wanapewa ushauri wa kitalamu zaidi katika masuala ya kilimo na ufugaji.


Naye Mwakilishi kutoka  Taasisi ya maendeleo ya jamii ya kusaidia vijana na kinamama(TAWESO) Fredy Julius alisema taasisi yao itaendelea kutoa mafunzo mbali mbali pamoja na kuwashauri wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika.


Aliwaomba wakulima kuacha kulima kilimo cha kizamani bali walime kwa kutumia mbegu bora na kujiunga katika vikundi mbali mbali vya wakulima.

Aidha kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa benki ya kilimo(TADB) tawi la Mwanza Marco Samson alisema benki yao itaendelea kutoa mikopo mbali mbali kwa wakulima ili wanufaike na kilimo.