TFF yawaita waonesha mpira kwenye vibanda


Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limewaita watu wote wanaoonesha mpira katika vibanda Jijini Dar es Salaam. Watu hao wameitwa kwa ajili ya kufanya kikao cha pamoja cha majadiliano ya ushirikiano, kitakachofanyika katika ofisi za shirikisho hilo, Karume katika manispaa ya Ilala.

Wamiliki hao wa vibanda vya kuonesha mpira wameombwa kufika kesho Jumanne, Agosti 27. Taarifa kamili ya TFF ni kama inavyoonekana hapa chini.