Timu za Jeshi Tanzania zazidi kujiweka sawa katika EAPCCO GAMES


Timu za Jeshi la Polisi Tanzania zikiwa katika mazoezi  katika viunga vya Chuo Kikuu cha Kenyata Jijini Nairobi nchini Kenya  baada ya kuwasili tayari kwa mashindano ya michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO GAMES), michezo inayofanyika Nchini Kenya.

Katika mashindano hayo, Jeshi la Polisi Tanzania linashiriki katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa kikapu, kareti, judo, taekwondo, vishale, riadha, kuvuta kamba na ulengaji wa shabaha. Mwaka jana 2018 michezo hiyo ilifanyika nchini Tanzania, ambapo Jeshi la Polisi Tanzania liliibuka mshindi wa pili katika matokeo ya jumla.