Loading...

8/13/2019

Uchumi wa Kagera unakuwa kwa kasi - RC Gaguti


Na Clavery Christian Bukoba

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jeneral E Marco Elisha Gaguti amesema kuwa uchumi wa mkoa Kagera unakuwa kwa kasi kubwa sana tofauti na hapo miaka ya nyumba hali ambayo imemfanya kuweka kongamano la wiki ya uwekezaji Kagera ambalo linalenga kutangaza zaidi fursa za uwekezaji zinazo patikana mkoani hupa.

Akizungumza na wafanyabiashara pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi ya Tanzania katika mataifa ya Kenya, Rwanda, Burundi, na DRC Congo amesema kuwa uchumi wa mwanchi wa Kagera umekuwa tofauti na miaka iliyopita, "Mwaka 2010 pato la mwananchi wa Kagera lilikuwa takribani Tsh, 667, 000 leo toka mwaka 2018 kwa takwimu zilizopo pato la mwananchi wa Kagera ni Tsh, 1300, 000 lakini pato jumla la mkoa limepanda toka Tsh, 1.3 tirion mwaka 2010 mpaka Tsh, 4.9 tirion mwaka 2018" Alisema Rc Gaguti.

Brigedia Jeneral Marco Gaguti amesema kuwa mkoa Kagera ni mkoa wa 24 kati ya mikoa 26 ambapo unachangia asilimia 3.6% katika pato la taifa ambapo amesema kuwa mbali na hayo mkoa Kagera umebahatika kuwa na fursa mbali mbali na unapakana na nchi nne za Africa ambazo ni karibu kupata wawekezaji wakuja katika mkoa wetu kufanya biashara na uwekezaji mbalimbali.

Aidha RC Gaguti amewashukuru mabolozi wanaowakilisha nchi ya Tanzania katika nchi za Africa mashariki kwa kuudhuria kongamano hilo ambalo linawapa nafasi wao kama mabalozi kuwaelezea fursa wafanyabiashara wa Kagera zinazopatikana katika maeneo yao.

Kwa upande wake balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dr, Pindi Chana amesema kuwa ni wakati mzuri sasa kwa wafanyabiashara wa mkoa Kagera na Tanzania kwa ujumla kutanua masoko ya nje ya nchi ili kuweza kukua kibiashara huku akiwasisitiza kuzingatia sheria na kanuni za nchi hasa katika swala la vibali na ubora wa bidhaa anayotaka kupeleka kuuza nje. Aidha Bi, Chana ameupongeza uongozi wa mkoa Kagera kwa kuliona hili na kuweka kongamano ambalo limekuwa laisi kwao kukutana na wafanyabiashara wengi kwa pamoja na kuwaeleza fursa zinazopatikana katika maeneo waliyopo huko nchini mwao.

Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania chini Rwanda, Burundi, Uganda na DRC Congo wamesema kuwa hali ya usalama katika nchi hizo ni swari kiasi kwamba ni raisi mtu kwenda kuwekeza na kupata faida huku wakiwashauri wakurugenzi walio na wilaya zinazopakana na nchi hizo kutumia mipaka hiyo kwa kuongeza pato la taifa kwa kujenga masoko ya pamoja miapakani hali itakayowawezesha watu wa nchi mbili kuuza na kununua bidhaa sokoni bila kuwa na usimbufu wa kuulizwa vibali na bila kuvunja taratibu za nchi husika.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger