Vipindi muhimu anavyopitia mwanadamu katika maisha

Kitaalamu binadamu katika safari ya ukuaji hupitia vipindi mbalimabali kama vile kuwa mtoto, kijana na uzee. Katika vipindi hivyo binadamu kwa muda mwingine huwa na furaha, huzuni, wasiwasi na hofu pia.

Vipindi hivyo ni;

Umri wa mwaka (0-18)
Katika kipindi hiki binadamu huwa mtoto na anyependwa sana na wazazi wake, katika kipindi hiki mwanadamu anakua kuwa katika kipindi cha  kufundishwa vitu kutoka kwa watu mbalimbali.
Mfano mtoto mdogo katika hali hii huwa kila amachokifanya kwake huona ni sawa eidha ni kinaya ama kizuri. Mzazi huchukua jukumu la kemkekemea kama anafanya jambo baya na humpongeza pale anapofanya vizuri mfano mtoto  hupongezwa  kumsaidia mzazi kufanya kazi, kuwaheshimu watu wote, kufauru katika masomo yake na mengineyo mengi. Kiujumla katika kipindi hiki binadamu huwa ni tegemezi kwa jamii inayomzunguka.

Kipindi cha umri kati miaka (19-35).
Katika kipindi hiki binadamu huanza kujitambua yeye ni nani. Vilevile katika kipindi hiki ni kipindi ambacho biandamu anaanza kupanga mipango mingi. Mfano katika kipindi hiki mtu huanza kupanga mambo mbalimbali nataka katika maisha yangu kitu cha kwanza kuwa nacho ni gari, mwingine utamsikia mimi nataka nianze kuwa na nyumba, wengine utasikia nataka kuolewa na mtu mwenye pesa, wapo wengine utawasika nataka kuoa mwanamke mzuri na mipango mingine mingi.

Katika kipindi hiki utawasikia  wanasema ndo kipindi cha kula ujana wakiwa na maana ya kwamba ni kipindi cha kwenda kumbi mbalimbali za burudani, pia ni kipindi cha kupendeza, pia ni kipindi cha vijana wengi kujiingiza katika kuiga mikumbo kutoka kwa watu mbalimbali hatimaye kujiingiza kwenye wizi, kuvuta bangi, umalaya na mengineyo mengi.

Utawasikia wengine wanakiita kipindi cha tumia pesa ukuzoee. Katika  kipindi hiki kina mambo mengi sana. Katika kipindi hiki tupo baadhi ya watu huwa bado wapo katika kipindi cha utegemezi. Mfano mzuri ni wanafunzi wanasoma elimu za juu yaani vyuo wao huamini ya kwamba hawawezi  kusimama wenyewe na kujitengeneze njia sahihi ya kujipatia kipato.

Pia wanafunzi hawa kwa walio wengi huwa wanafikiri maisha baada ya elimu zao ni kuajiriwa pekee yake. Lakini ndugu msomaji wa makala hii lazima ufikiri zaidi kuajiriwa peke yake ili uweze kuona mafanikio makubwa ndani yako. kitu kikubwa ni kuwa mbunifu. Wito wangu kwako ni kwamba endapo utatumia vizuri kipindi hiki ukiwa na mtazamo chanya utapata mafanikio makubwa sana.

Umri kati miaka (36-45).
Ni aina nyingine ya vipindi ambayo hupitia mwanadamu. katika kipindi hiki ni kipindi cha utekelezaji wa   yale uliyoyapanga katika kipindi ulichopita yaani cha miaka( 19-35). Katika kipindi hiki  ni kipindi ambacho kina majukumu mengi ambayo yanamfanya mtu akose hata usingizi. Katika kipindi hiki mtu huwa na majukumu mengi sana kwa mfano kujenga,kusomesha watoto,huenda ukawa tegemeo katika familia yako.

Kwa kuwa katika kipindi hiki kina mambo mengi ya utekelezaji ni vema kile unachokipanga katika kipindi cha mipango yaani miaka (19-35) na utekelezaji uanza katika kipindi hicho. Nasema hivi nikiwa na maana ya kwamba katika kipindi hiki  cha miaka 36-45 watu wengi hujikuta wana mipango mingi lakini ugumu unakuja katika utekelezaji.

Umri kati ya miaka 46-nakuendelea
Hiki ni kipindi cha uzee ambacho mara nyingi huiitwa ni kipindi cha masahihisho. Katika kipindi hiki baadhi ya watu hupungua uwezo wa kufikiri hatimaye kuwa kama watoto. Pia Watu wengi hapa hupatwa na magonjwa mbalimbali kama pressure,figo kufeli, kisukari n.k. Katika kipindi hiki watu hustaafu kazi zao.

Katika kipindi hichi watu wengi hupatwa na psessure kutoka walishindwa kupanga na kutekeleza mambo yao katika vipindi vya umri kati (19-35). Mfano mtu alikuwa ni mfanyakazi wa serikali na hajawahi kujenga nyumba yake ya kuishi wala  hana usafiri vyote alivyokuwa anatumia vilikuwa ni mali za ofisi.

Inapofika wakati wa kustafu anapata mafao yake ndo pale anaanza kupanga mipango yange na kujikuta hela aliyopewa katika kiuna mgongo imeisha kwa sababu mtu huyu anakuwa ana mipango mingi katika kipindi cha uzee matokeo  haelewi aanze na kipi katika utekelezaji je aanze na kununua gari? Je aanze na kufungua biashara? Je aanze na kujenga nyumba? Matokeo yako mipango inakuwa mingi kuliko utekelezaji hatimaye anapata pressure.

Wito wangu kwako kumbuka siku zote  kupanga ni kuchagua na kutenda ni kuamua. Katika safari ya mafanikio kila linalowezekana leo lisingoje kesho. Ewe kijana tambua ya kwamba muda wa kupanga na kutekeleza mambo yako ni sasa achana na usemi eti kijana ni taifa la kesho kwa kuwa  ukiushika usemi  huo utakuwa unachelewa katika  safari yako mafanikio.

Muubgwana inakutakia kila jema katika safari yako ya mafanikio. Pia endelea kutembelea  ukurasa huu kila siku ili ujifunze zaidi kuhusu mbinu mbalimbali za mafanikio.

Na. Benson Chonya